16/12/2011

SOMA CHUO CHA HAVARD BURE

Usishutuke na wala sio utani. Tunaweza kweneda havard  na kusikiliza lekcha bila wewe kupanda ndege. Gharama utayotumia ni  ndogo sana. Ukisikia dunia imekuwa kama kijiji ni sababu na  faida na Fursa zinazoletwa na TEKNOHAMA

15/12/2011

NDANI YA KIWEKA DATA(HDD) KUNANI

Siku chache zilizopoita katika forum maarufu ya ya jamii forum kuna mjumbe aliwasilisha tatzo la HDD yake. Tatizo lile lililifanya na lilinipa nguvu ya kufanya kitu ambacho nilipanga kukifanya sikuuuuu nyingi lakini sikuwa na mwammko au muda. Ni kitu gani hicho??? Ni kuangalia kuna vitu gani ndani ya Hard  Disk  Drive (HDD)
Katika makororo yangu ya kompyuta nilikuwa nina HDD ya Maxtor ya 20GB amabayo ilikwua mbovu. Zaidi ya HDD kilichohitajika  kingine ni screw driver sahihi.
Yafuatayo ni maelezo ya picha nilizopiga mwenyewe na ufafanuzi wa sehemu mbali mbali za HDD. Kumradhi kwa quality duni ya picha lakini ni matumanini yangu ujumbe uliokusudiwa utaelewekwa bila tatizo
Kwanza tunaaza kufungua screw zinazoshiikilia kasha
Mara nyingi HDD zina rangi ya shaba. Juu ya HDD kuna maelezo mbali mbali mbali kama y size, Pembeni kuna Seheumu za HDD kupokea moto kutoka kwneye Poer supply. Pia kuna waya (Data bus) ya kupokea datakutka na wenda kwenye motherboard.  HDD Inaweza kuwa ni ya IDE au SATA.
Srew nyingine zimefichwa
Katila kuhakikisha kuwa wanagundua  mtu akikiuka masharti ya wararty kuna srew nyingine zinafichwa chini ya label . Kufungua azima uchane label. Ukichana label then warannty hakuna . Hii ni HDD mbovu tunaendelea. Katika picha hii kwenye HDD unaweza uona kuna malezo mengi juu ya HDD husika.Kuna maelezoni jinsi gani HDD inaweza kufanywa kuwa master au Slave.

HDD circuit board aka motherbard ya HDD
Circuit board hii ndio ubongo wa HDD inayoongoza utendaji kazi wa vifaa mbai mbali ndani ya HDD.  Nimeipachika jina la motherboard ya HDD .Hapa ukifungua screws zilizoshikilia ubao huu basi unaweza utenganishwa na kasha la Hard Disk
Mawasiliano ya Circuit board na HDD
Kilichoishangaza hakuna waya waya  zinazounganisha HDD na  circuit board. Mawasiliano  yanafanyika kutumia vitu kama spring.Waliobobea wenye mamb ya electoniki wanaweza kujua sababu ya hili. Tunaweza kuuuliza pia kwa nini circut board zinakuwa na rangi ya kijani?

Platters and Read/Wrte heads
  Ganda la HDD likiondolewa  tunaona kitu kama kisahani(platter) Hii ndio disk yenyewe. Pia kuna  kichwa chakusoma na kundika data kwenye kisahani. Kwa jina la kitaalam kinaitwa Read/Wite heads. Kisahanikinangara   sana na  inashauriwa  kazi hii ifanyike kwenye chumba kisafi sana. Kama nilivyosema sijali sana sababu hii ngoma ilishaharibika siku nyingi

Mkono wa kuandika na Kusoma

Na hapa  ndio electroniki za “mkono” unaotmika kuanidka na kusoma data kutoka na kwenda kwenye kisahani zilipo. kumbuka utendaji kazi wa haya yote unaogozwa na na circuit board.
Kwa leo tuishie hapo . Tutavipingua zaidi vifaa vingine siku nyingine. Kama una chochte cha kuongeza kupunguza kuponda  usisiste kuacha maoni