17/11/2011

Sifa za mwanateknik bora

Moja kwa moja kwenda hoja .Haya ni baadhi ya mambo yanayoweza kufanya mtu yeyote kuwa katika nafasi ya kujiita mwanateknolojia bora mwenye taarifa sahihi na za wakati.natarji wazefu  wataongeza zaidi

1. Jifunze jambo au habari mpya kila siku.

Kwa kutumia gooogle na mitandao mbali mbali mbali ni rahisi kujifunza mambo mapya ya kitenolojia. Changamoto ni chanzo ni chanzo na habari gani hasa zina mafunzo. Kutokana na uelewa , fani tofauti watu tuna prority tofauti
Mfano zaidi ya jf tovuti nyingine ambazo binafsi natumia kujifunza na kupata tech news ya issue mbali mbali ni Dailytech, Techcrunch, Click Online
Cha msingi watu tuelewe internet ina kila aina ya habari nzuri na ina kila aina ya habari za ajabu. Mfano nimeona hapa kuna baadhi ya member wanapost article za kuhusu virus amabazo sio za kweli.(Hoax) Ujumbe unaasema eti virus ataburn the whole HDD. Hivi kuna virus anaweza kuunguza HDD.??????. So tusiamini na kucukua kizima kizima kila tunachoona kwenye net. Some time tuchunguze na tujirizishe.

2. Fanyia kazi na jaribu mambo kwa vitendo

Binafsi naona watanzania wengi tumeridhika na utaalam wa theory. Ikija kwenye nadharia na vitendo tunakwama na kukutana na vikwazo vingi. Hii inatokana na watu kuridhika nadhiria kitu amabcho si kizuri sana. Kifupi hatupendi kupigika. Ninafanya kazi na mtu ambaye hapendi kuonekana kashika cripping tool. Alanachukia kweli kuitwa fundi au techinician Teh teh teh. Yeye anataka aitwe Network admin au engineer.
Mwisho wa siku tunakuwa na vyeti safi lakini hatuna good practical experince………….


3. Jiulize na uliza maswali magumu

Kuna wataalamu hawapendi au wanaona aibu kuonekana wanauliza maswali .Binafsi naamin tutakuwa watalmu bora kama tutakubali kuwa una wakati tunaweza kuwa “wanafunzi” na kuna wakati tunaweza kuwa “walimu”. Pausing kama mwalimu tuuuu au kama mwanafunziii tuuuuuuu siku zote haiwezi kumjenga mwanateknolojia. Na hata wanasiasa..
Jiulize zaii di na zaidi
maswali magumu
Chimba zaidi uelewe zaidi
Mfano una watu nimeona wanajiuliza maswali ya kuchakachua TV decoder ili wapate channel za bure. Lakini sio wengi wa watu hawa wamejiuliza swali gumu kwanza la HowStuffWorks “Satellite TV System”.. Mtu akisoma articles mbali mbali kuhusu hili anaweza kujua urahisi na ugumu wa kuchakachua channel na atauwa kajifunza.

Tofauti ya DVD na CD ni Nini? Haraka haraka jibu ni kwamba DV ina size kubwa. Lakini tuendelee tjaribu kujiliza swali gumu. Kwa nini DVD ina uwezo mubwa wa space na C ina uwezo mogo waati kimaumbile zote ni sawa? . Kwa hiyo tujaribu kchimba na kuelewa kiundani. La sivyo tutajikuta tunajiita wataaam tunatoa maelezo amabayo sio ya kitaalam.
Mtu akikuuliza kama mtaalam unajirate vipi utaalam wako wa iwe ni ICT, umeme programming, etc .? Wewe ni Advanced, Avarage or just end user. Binafsi i treat myself an avarage but competent ICT techician.

4. Penda majadiliano endelevu

kuna baadhi ya watuu hapa kwenye teknoloja na hata huko kwenye siasa na majukwaa mengine hawapendi kutoafautiana kwa mawazo, approach na ideas.. ..Ukimkosoa kitu anakuona adui au anakuwa mkali Vile vile kuna wale wengine kwa kuwa wajua sana akiona mtu anafanya au kaandika kitu fulani anamponda. Tena mbaya zaidi kwa lugha ya dhiaki.

Majadiliano
Mijada ni muhimu katika kukuza ujuzi
Tunachotakiwa kufanya ni simple kwanza tukubali kutaofautina na pili tukubali na tukaribishe majadiliano endelevu kwa lugha nzuri..



5. Wezesha end user kutatua matatizo yao wenyewe

Kuna watalaam wanapenda kuendelea kutatua matatizo madogomadogo badala ya uwaambia wahusika nini cha kufanya wenyewe. huu unaweza kuwa ni uchoyo na vile vile kuna watu hawapendi kufuata proceure kusoma manual ya vifaa vyao huu nao ni Uvivu mbaya. So upande wa wataalam ni vizuri kuwawezesha watu kutatua matatizo madogo madogo ili wasisumbe tena na upande wa watuamiji wa kawiada uipta tatizo soma manual yakifaa au tafuta manua ya kifaa mtandaoni.
Tegua kitedawili: Je dereva asiyependa kuchafuka lakini anaelewa vema kueleazea kila kifaa cha gari yake ni mwanateknolojia bora Kuliko fundi anayealitenegza gari hilo kila likiharibika?
Je kuna jambo nimeliacha, nimekosea au sijaligusia?usisite kunikosoa kuongeza au hata kuchakachua…..

No comments:

Post a Comment